John 14:1-6

Isa Awatia Moyo Wanafunzi Wake

1 aIsa akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 bNyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Naenda kuwaandalia makao. 3 cNami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.”

Isa Ndiye Njia Ya Kwenda Kwa Baba

5 dTomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?”

6 eIsa akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
Copyright information for SwhKC